Alama za huzuni na majonzi zimetanda katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kuhuisha kifo cha kiongozi wa wakweli na Imamu Jafari Swadiq (a.s).
Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu kwa kushirikiana na watumishi wa kitengo cha ushonaji chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya, wameweka mapambo meusi katika Atabatu Abbasiyya na vitambaa vilivyo andikwa maneno ya huzuni na kuomboleza pamoja na baadhi ya hadithi kutoka kwa muombolezwa.
Aidha zimewashwa taa nyekundu zinazo ashiria huzuni na majonzi, swala hilo linaenda sambamba na ratiba ya uombolezaji iliyoandaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, katika msiba huu mkubwa kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wapenzi wao, tukio hili hufanywa kila mwaka mwezi ishirini na tano Shawwal.
Kumbuka kuwa mwezi ishirini na tano Shawwal mwaka wa (148h), alikufa kishahidi Imamu Swadiq (a.s) akiwa na umri wa miaka (65), alifanyiwa dhulma na udhalilishaji mkubwa kutoka kwa watawala wa Bani Ummayya, kisha watawala wa bani Abbasi, akauliwa (a.s) kwa sumu na mtawala wa Bani Abbasi aitwae Abu Jaafari Mansuur.