Kitengo cha Dini kwa kushirikiana na kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya majlisi katika ukumbi wa utawala, kuomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s), iliyohudhuriwa na watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kundi la mazuwaru.
Majlisi zimefanywa kwa muda wa siku mbili na kuhitimishwa asubuhi ya leo Ijumaa, zilikua zinafunguliwa kwa Qur’ani tukufu na kufuatiwa na mawaidha yaliyokua yanatolewa na Shekhe Muhammad Kuraitwi, alikua anaongea kuhusu Maisha ya Imamu Swadiq (a.s), sambamba na kueleza elimu, upole na subira aliyokua nayo, na jinsi alivyofanikiwa kufikisha ujumbe wa babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwa umma wake.
Akaeleza ugumu wa mazingira aliyoishi, pamoja na ugumu huo aliendelea kutoa elimu wakati wa kipindi cha Uimamu wake kilicho dumu kwa miaka telathini na nne baada ya baba yake (a.s), akaweza kulinda madhehebu tukufu ya Ahlulbait (a.s).
Majlisi zilikua zinahitimishwa kwa kusomwa tenzi za kuomboleza zenye maneno ya huzuni kutokana na msiba huo.