Watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaomboleza kifo cha Imamu Swadiq mbele ya malalo ya babu yake na Ammi yake (a.s)

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya siku ya Ijumaa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya matembezi ya uombolezaji, katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s), wamekwenda kumpa pole babu yake Imamu Hussein na Ammi yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Matembezi yao yameanzia ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), walianza kwa kufanya majlisi ya kuomboleza msiba huo, kisha wakaanza kutembea na kuelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), wakipita katika uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu, walipo wasili kwenye haram ya bwana wa vijana wa peponi Imamu Hussein (a.s) wakapokewa na maukibu ya watumishi wa Atabatu Husseiniyya, kisha wakafanya majlisi ya pamoja ndani ya haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) iliyopambwa na tenzi na mashairi kuhusu msiba huo, na athari kubwa aliyoacha katika umma wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na misingi ya Dini ya kiislamu.

Kumbuka kuwa brogram ya uombolezaji ni sehemu ya utaratibu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwenye kila tukio la kumbukumbu ya kifo cha mtu miongoni mwa watukufu wa nyumba ya mtume hufanywa matembezi maalum ya uombolezaji kuanzia Atabatu Husseiniyya hadi Atabatu Abbasiyya au kinyume chake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: