Sayyid Swafi amzawadia mcheza filamu iliyoshinda kwenye kongamano la kimataifa lililofanywa Baabil

Maoni katika picha
Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amemzawadia mcheza filamu ya (Al-khilaasu), iliyoandaliwa na kituo cha Aljuud katika kitengo cha Habari cha Ataba tukufu, ambayo imekua miongoni mwa filamu tatu zilizo shinda kwenye kongamano la sinema lililofanywa Baabil (Babel Film Festival for Animation) awamu ya tatu.

Mkuu wa kituo cha Habari, Ustadh Ahmadi Twalibu Abdul-Amiir ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Zawadi imetolewa mbele ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Dhiyaau-Dini, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria, mkuu wa kitengo cha Habari, rais wa kitengo cha Habari, viongozi wa kitengo cha teknolojia ya mitandao pamoja na kundi la watumishi wa kituo”.

Akabainisha kuwa: “Zawadi hiyo ni sehemu ya msaada wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu na viongozi wake, hususan sekta ya teknolojia, jambo ambalo limepelekea ushindi wa kazi hiyo katika shindano lililokua na kazi zaidi ya (30) kutoka nchi (16) za kiarabu na kiajemi zilizo shiriki kwenye kongamano hilo”.

Akasisitiza kuwa: “Mheshimiwa Sayyid amesifu mafanikio hayo na akahimiza watumishi waendelee kufanya vizuri, kwa kutoa mawazo yanayo endana na misingi ya Dini na jamii, katika wakati ambao tunashuhudia watu wanafanya kazi zisizoendana na maadili ya raia wa Iraq”.

Kumbuka kuwa filamu iliyopata tuzo imetengenezwa na watumishi wa kitengo cha habari kilicho chini ya Ataba tukufu, ilikua inahusu mazingira halisi waliyoishi raia wa Iraq baada ya kuvamiwa na magaidi wa Daesh, na namna raia hao walivyo itikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kulinda taifa la Iraq na maeneo matakatifu, ikafafanua moyo wa uzalendo na hamasa waliyonayo wananchi wa taifa hili, ambao wamepambana vita kali mmno katika historia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: