Majlisi ya kuomboleza kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya, kimefanya majlisi ya kukumbuka kifo cha Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s).

Mkuu wa kituo bibi Zainabu Ardadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Majlisi ni sehemu ya ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika tukio hili, imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, yakafuata mawaidha elekezi kutoka kwa mhadhiri wa mimbari ya Husseiniyya Zainabu Hassan, ameongea kuhusu (Kuchunga nafsi) akataja hatua muhimu za Maisha ya Imamu Maasum (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya hapo zikasomwa tenzi na kaswida za kumpa pole Imamu wa zama, majlisi imehitimishwa kwa kusoma dua ya Faraj ya kuharakisha kudhihiri kwa Qaaid Aali-Muhammad (a.f)”.

Akasema kwa: “Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya hufanya kila iwezalo katika kutumikia mimbari ya Husseiniyya na majaalisi tangu kuanzishwa kwake hadi leo, wameshukuru ushirikiano wa kweli uliopo katika kuhuisha matukio mbalimbali ya Ahlulbait (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: