Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu leo siku ya Jumamosi, kimefanya hafla ya kuanza kuwajibikiwa kisheria kwa kundi la wanafunzi wa shule za Al-Ameed/ wavulana.
Hafla hiyo imefanywa katika jengo la Shekhe Kuleini chini ya kauli mbiu isemayo (kwa kuwajibika kwangu nakua bora), imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini, jopo la wajumbe wa kamati kuu, marais wa vitengo na viongozi wa idara.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na msomaji wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Haidari Jalukhani, halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukasikilizwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Ibaa).
Ukafuata ujumbe kutoka kitengo cha malezi na elimu ya juu ulio wasilishwa na makamo rais wa kitengo tajwa Dokta Hassan Daakhil, akasema: “Kundi jipya la wanafunzi wa shule za Al-Ameed miaka yao imewaruhusu kuingia kwenye mlango wa kuwajibikiwa kisheria kati ya mja na Muumba wake”.
Akaongeza: “Kufanya hafla hii -kwa mtazamo wetu- ni sehemu ya wajibu wetu, kwani vijana wanatakiwa kupewa uwelewa sahihi, sio kwamba wanaingia kwenye uhuru usiokua na mipaka, hafla hii inawakumbusha majukumu waliyo nayo na umuhimu wa kujiandaa kwa ajili ya kudumisha mawasiliano kati yao na Muumba wao”.
Akaendelea kusema: “Hafla hii sio jambo dogo, bali ni ratiba kubwa na muhimu, inaacha athari katika maisha ya vijana wetu, na kuwa chachu ya kutekeleza mafundisho ya Dini yao tukufu, sambamba na mazingira mazuri ya shule yanayo wakumbusha wajibu wao binafsi na kijamii”.
Akamaliza kwa: “Kutoa shukrani za dhati kwa kila aliyechangia kufanikiwa kwa hafla hii, akawashukuru wazazi wa vijana hao kwa ushirikiano mkubwa waliotoa katika kupanda misingi ya Dini tukufu kwenye nafsi za watoto na wanafunzi wetu”.
Hafla imepambwa na igizo lililofanywa na kundi la wanafunzi waliofanyiwa hafla, igizo limepambwa na beti za tenzi na mashairi.
Hafla ikahitimishwa kwa tukio la pamoja lililo andaliwa na idara inayoratibu na kusimamia hafla za kuingia umri wa kuwajibikiwa kisheria.