Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya majlisi ya kuhuisha kifo cha mkweli wa familia Imamu Jafari Swadiq (a.s), ndani ya ukumbi wa jengo la utawala na kuhudhuriwa na rais wa chuo hicho Dokta Nurisi Dahani na kundi la walimu na watumishi.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Sayyid Muhandi Almayali mkuu wa Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu, yakafuata mawaidha yaliyotolewa na Shekhe Abdullahi Dujaili, ameongea historia ya Imamu Swadiq (a.s), pamoja na changamoto kubwa aliyokua nayo lakini aliweza kufikisha ujumbe wa baba zake (a.s), ambao ni muendelezo wa ujumbe wa babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), akatoa wito wa kufuata mwenendo wake mtukufu na hadithi zake.
Majlisi ikahitimishwa kwa tenzi na mashairi kuhusu kisa cha kuuawa kishahidi kwa Imamu (a.s), pamoja na dhulma alizo fanyiwa wakati wa uhai wake.
Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kimezowea kuhuisha matukio yanayohusu watu wa nyumba ya Mtume (a.s), kuanzia matukio ya kuzaliwa na kufariki, na hualika wasomi na wahadhiri mahiri.