Idara ya usomaji wa Qur’ani chini ya Maahadi ya Qur’ani tukufu, imefanya semina ya hukumu za usomaji wa Qur’ani, sauti na naghma kwa mahadhi ya kiiraq na kimisri kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Jumla ya watumishi (30) kutoka vitengo tofauti wameshiriki kwenye semina hiyo, wanafundishwa kwa nadhariyya na vitendo, mkufunzi ni Ustadh Alaau-Dini Hamudi kiongozi wa idara ya usomaji.
Washiriki wanafundishwa sauti kwa mahadhi ya kiiraq na kimisri na mkufunzi wa mahadhi hayo ni Uatadh Haidari Jalukhani Mussawi.
Tambua kuwa semina itadumu kwa muda wa mwezi mzima, kutakua na mitihani ya nadhariyya na vitendo kwa lengo la kupima uwezo wa washiriki, na kujenga uwezo wao kwa kuwapa nafasi za kushiriki kwenye semina zijazo, na kuendelea kunufaika nao kwenye miradi ya Qur’ani inayofanywa na Maahadi.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni sehemu ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inalengo la kueneza elimu ya Qur’ani na kuandaa jamii yenye uwelewa wa Qur’ani tukufu kwenye sekta tofauti.