Kuhitimu kwa semina tatu za Qur’ani katika Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya kuhitimu wanafunzi (35) wa semina tatu za njia ya mtandao, ambazo ni: (Semina ya Bayyinaat, semina ya bibi Khadija (a.s) na semina ya Safinatu-Nnajaa).

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jawadi Aljaburi amesema: “Mwenyezi Mungu mtukufu ametuwezesha kuwatahini wanafunzi (35) waliosoma hukumu za tajwidi na usomaji sahihi wa Qur’ani kwa njia ya mtandao”.

Akabainisha kuwa: “Semina hizi zinamuandaa mshiriki kuingia kwenye hatua ya kuhifadhi Qur’ani tukufu”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya inafanya kila iwezalo kuandaa kizazi cha wanawake wasomi wa Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: