Majeruhi kutoka wizara ya mambo ya ndani wanaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kugharamia matibabu yao

Maoni katika picha
Kundi la majeruhi kutoka wizara ya mambo ya ndani wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kugharamia matibabu yao na kuwapa viti-mwendo vya kisasa kupitia hospitali ya rufaa Alkafeel.

Majeruhi hao wametoa shukrani zao walipokwenda kufanya ziara kwenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), wakasifu kazi zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya chini ya kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Swafi, wakasema kuwa hakika Atabatu Abbasiyya imekua mstari wa mbele daima katika kusaidia majeruhi na familia za mashahidi.

Mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel Ustadh Muhammad Haadi akasema kuwa: “Kuna awamu nyingine ya kugawa viti-mwendo itakayo fuata, kutokana na agizo la Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi”.

Akaendelea kusema: “Majeruhi wetu wa leo wametoka mikoa tofauti, kuna waliotoka Nainawa, Ambaar na mikoa mingine”. Akafafanua kuwa: “Jambo hili ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kuwajali majeruhi na kuwapa kila aina ya msaada”.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, inaendelea kutibu majeruhi wa jeshi la serikali na Hashdu-Sha’abi, na Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka swala la kuhudumia majeruhi na familia za mashahidi katika vipaombele vyake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: