Bidhaa za Khairul-Juud.. zimekubalika sana kwenye maonyesho ya kimataifa yanayofanyika Basra

Maoni katika picha
Shirika la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Kharul-Juud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, bidhaa zake zimekubalika sana kwenye maonyesho ya kibiashara yanayo endelea hivi sasa kwenye uwanja wa bandari ya Muaqal mkoani Basra.

Mhandisi Falahu Fatliy kiongozi wa idara ya masoko na mauzo ya shirika ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika shirika letu likomstari wa mbele daima katika kushiriki kwenye maonyesho na makongamano ya kibiashara, sambamba na kuwa karibu na watumiaji wa bidhaa zetu na kusikiliza maoni yao kuhusu bidhaa, na kuwaletea karibu kile wanacho hitaji kutoka kiwandani moja kwa moja”.

Akaongeza kuwa: “Tawi letu linabidhaa tofauti za nyumbani, viwandani na hospitalini, zenye ubora wa hali ya juu kwa mujibu wa shuhuda za watumiaji wa bidhaa zetu, aidha bidhaa zetu zinakidhi mahitaji ya watumiaji na zinatoa ushindani mkubwa kwa bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vingine kwenye soko, jambo hili linatokana na kazi nzuri inayofanywa na watumishi wa shirika ya kutengeneza bidhaa zenye ubora mkubwa zinazo uzwa kwa bie ndogo”.

Familia nyingi za wakazi wa Basra na watu wanaotembelea maonyesho haya wamepongeza bidhaa zinazo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud, kwani zinaumuhimu mkubwa katika soko la ndani, ubora wake unazidi bidhaa zinazo toka nje ya nchi na zinauzwa kwa bei nafuu.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya imeshiriki kwenye maonyesho haya ikiwa na mashirika tofauti, miongoni mwa mashirika hayo ni hili la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Khairul-Juud, shirika la uchumi Alkafeel, Darul-Kafeel ya uchapaji na usambazaji, shirika la bidhaa za chakula na wanyama Nurul-Kafeel, mashirika hayo ni kielelezo cha uwezo wa Iraq kwenye sekta ya viwanda, aidha ni fursa ya kubadilishana uzowefu na mashirika mengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: