Ugeni kutoka chuo kikuu cha Tehran nchini Iran umesema: Tunajitahidi kujenga ushirikiano wa kielimu, kitamaduni na kubadilishana uzowefu na chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nuris Muhammad Shahidi Dahani, akiwa na makamo wake wa taaluma, wakuu wa vitivo na wasaidizi wao, wamepokea ugeni kutoka chuo kikuu cha Tehran Iran, walio fanya ziara yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kielimu na kitamaduni baina ya vyuo hivyo.

Dahani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mlango wa chuo uko wazi kwa yeyote kutoka ndani na nje ya Iraq, tumekua tukipokea wageni tofauti wakiwemo wageni hawa, tumewaambia malengo ya chuo na mtazamo wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika mradi wa malezi na elimu, na huduma zinazo tolewa na Ataba kwenye sekta ya elimu kwa lengo la kutumikia jamii”.

Naye rais wa ugeni huo Profesa Muhammad Hassan Swadiqi akauambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumefanya ziara hii kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano wa kielimu, kitamaduni na kubadilishana uzowefu baina ya vyuo vyetu, tumefanikiwa kuangalia kumbi za madarasa ya chuo kikuu cha Alkafeel na maabara yao, bila kusahau eneo la bustani na miradi ya baadae, hakika tumeona maendeleo makubwa na mazingira mazuri ya usomaji”.

Mwisho wa ziara hiyo ugeni umemshukuru sana rais wa chuo kikuu cha Alkafeel na viongozi wenzake kwa kusimamia vizuri miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wakatoa wito kwa uongozi wa chuo kikuu cha Alkafeel ukatembelee chuo kikuu cha Tehran.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: