Idara ya Qur’ani chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuanza awamu ya pili ya semina ya Yanaabia-Rahmah ambayo usajili wake umefanywa siku chache zilizopita.
Kiongozi wa idara bibi Fatuma Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Semina awamu ya pili inafanywa chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kutumia kipindi cha likizo za majira ya joto kuendesha program mbalimbali zinazo endana na umri wa washiriki ambao ni miaka (14 na 15)”.
Akaongeza kuwa: “Kutokana na wingi wa washiriki na kwa ajili ya kufaidisha kundi kubwa zaidi, wanafunzi tumewagawa kwa zamu za wiki mbili kila kundi na tumeandaa ratiba yenye masomo yafuatayo (Fiqhi – Aqida – Visa vya Qur’ani – Kazi za mikono – Hukumu za usomaji – Tafsiri – Utamaduni wa kiislamu), pamoja na vipindi vya michezo na mashindano”.
Akabainisha kuwa: “Siku ya kwanza tumefanya ukaribisho na ufunguzi wa semina kwa usomaji wa pamoja wa surat (Yaasin), kisha ikasomwa ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuongea kuhusu kumbukumbu ya mazazi ya bibi Maasumah (a.s), halafu washiriki wakatembelea makumbusho ya Alkafeel”.
Kumbuka kuwa hii ni miongoni mwa semina nyingi ambazo hufanywa, mahitaji yote yameandaliwa, ikiwa ni pamoja na usafiri wa kwenda na kurudi, zawadi kwa watakaofanya vizuri na vyeti vya ushiriki.