Maahadi ya Alkafeel ya watoto wanaoweza kusoma inafanya semina kuhusu namna ya kupambana na majanga ya moto

Maoni katika picha
Maahadi ya Alkafeel ya watoto wanaoweza kusoma inafanya semina ya watoto wanaoweza kusoma, inahusu mbinu za kupambana na majanga ya moto na namna ya kutumia vifaa vya zimamoto.

Semina imefanywa kwa kushirikiana na idara ya mitambo ya tahadhari na zimamoto, chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa lengo la kujikinga na majanga ya moto na kuwafanya watumishi kuwa tayali kupambana na moto wakati wowote ukitokea -Allah atuepushie-.

Semina imefafanua kwa upana aina za moto na namna ya kutokea kwake, sambamba na namna ya kuweka kinga ya moto kila sehemu, kwa kufanya baadhi ya mambo ambayo huzuwia kuwaka moto.

Tambua kuwa Maahadi ya Alkafeel ya watoto wanaoweza kusoma, hutoa huduma mbalimbali katika mkoa wa Karbala na Iraq kwa ujumla, wakufunzi wake wanauzowefu wa miaka kumi na moja, huduma zoto hutolewa bure, sambamba na kusaidia kundi la watu wenye mahitaji maalum kwa kuwapa mafunzo mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: