Kuanza usajili wa awamu ya sita ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Qur’ani katika Majmaa ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuanza usajili wa washiriki wa mradi wa kiongozi wa wasomi wa kitaifa awamu ya sita, usajili utaendelea hadi (6 Juni 2022m).

Masharti ya kujiunga mwaka huu ni:

  • - Maombi rasmi yatafanywa kwa njia ya mtandao kupitia link ifuatayo (https://forms.gle/HGSYgdus7DsQS1bd7) au kuskan barkod.
  • - Kwa ajili ya kurahisisha ushiriki mwaka huu, kamati ya maandalizi imeamua mtihani wa majaribio utafanywa kwa utaratibu ufuatao.

Kwanza: Mshiriki atume rekodi yake aliyosoma sehemu yeyote ndani ya Qur’ani (kwa mahadhi ya kiiraq au mimisri), kwa muda wa (dakika moja na nusu hadi dakika mbili), katika usomaji wake azingatie maswali na majibu.

Pili: Rekodi hiyo iwekwe kwenye fomu ya kimtandao (kipande cha video ya muombaji), aandike majina yake matatu na jina la mkoa anaoishi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba ya siku ifuatayo: (009647692343344).

Kumbuka kuwa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa husimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, unalenga kuandaa na kuendeleza vipaji vya usomaji wa Qur’ani hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: