Ugeni kutoka jamii ya Bohola umetembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kukutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini.
Ugeni huo unaongozwa na muwakilishi mkuu wa Bohola nchini Iraq Shekhe Idirisa Abdullahi Burhani, mkutano huo umehudhuriwa pia na mjumbe wa kamati kuu Ustadh Huquqi Kaadhim na baadhi ya marais wa vitengo, wamejadili baadhi ya huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru ndani na nje ya Iraq, sambamba na kusikiliza maolezo kuhusu baadhi ya miradi ya Ataba.
Mwisho wa ziara hiyo na kikao hicho, wageni wamepongeza sana huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya usimamizi wa kiongozi mkuu wa kisheria na katibu mkuu pamoja na watumishi wao, wakamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awadumishe katika kazi hiyo.