Wanafunzi wa mradi wa Qur’ani Alkafeel wanafanya mtihani wa mwisho

Maoni katika picha
Wanafunzi wa mradi wa Qur’ani Alkafeel, unao endeshwa na Maahadi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, wanafanya mtihani wa nadhariyya wa mwisho katika mada ya kusimama na kuanza.

Mtihani huo umefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya na kushiriki idadi kubwa ya wanafunzi wa mradi huo.

Mtihani unalenga kupima kiwango cha washiriki na kutambua tofauti baina yao kwenye masomo waliyofundishwa wakati wote wa semina.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni sehemu ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, yenye jukumu la kufundisha Qur’ani na kuandaa jamii ya wasomi wa Qur’ani katika kila sekta.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: