Mahafali ya Mimbari za Nuru katika mkoa wa Waasitu

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya vikao vya usomaji wa Qur’ani katika mkoa wa Waasitu.

Mahafali hiyo imefanywa ndani ya chuo kikuu cha Ausi kwa kushirikiana na umoja wa wasomaji wa Qur’ani, pamoja na kikundi cha Answaru-Marjaiyya katika wilaya ya Kuut, wamehudhuria wasomaji maarufu wa Qur’ani, wapenzi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu, viongozi wa Dini na taasisi zinazojishughulisha na Qur’ani hapa mkoani.

Masikio ya wahudhuriaji yameburudishwa kwa aya za Qur’ani tukufu zilizosomwa na Haidari Muhsin Abazuni, msomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu Ammaar Alhilliy, pia msomaji Mustwafa na muwakilishi wa umoja wa wasomaji wa Qur’ani katika mji wa Waasitu, mahafali imepambwa kwa beti za mashairi ya kuwapenda Ahlulbait (a.s).

Kumbuka kuwa mradi wa Mimbari za Nuru unalenga kufanya mahafali za usomaji wa Qur’ani tukufu ndani na nje ya mkoa wa Karbala, kwenye Ataba, Mazaru, Husseiniyya na Misikiti, kwa kushirikiana na taasisi zinazojishughulisha na Qur’ani kwenye maeneo ambako mahafali za usomaji wa Qur’ani zinafanywa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: