Kiongozi mkuu wa idara ya utunzaji wa mazingira ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa idara ya utunzaji wa mazingira katika eneo la Furaat, ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu akiwa na baadhi ya wajumbe aliofuatana nao.

Wamefanya ziara mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kisha akakutana na rais wa kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Huquqi Muhammad Ali Azhar.

Baada ya kukaribishwa ugeni huo wamejadili mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru, na mchango wake katika utunzaji wa mazingira na miradi yenye uhusiano na jambo hilo sambamba na namna ya changamoto ya uchafuzi wa mazingira unaoshuhudiwa hapa nchini.

Mwisho wa ziara wageni wakashukuru Atabatu Abbasiyya na watumishi wake kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhudumia mazuwaru, na miradi inayosaidia juhudi za serikali kwenye nyanja tofauti, ikiwa ni Pamoja na upande wa mazingira.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: