Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Shimri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Nadwa imefanywa ndani ya ukumbi wa Shekhe Answari katika jengo la Imamu Murtadhwa (a.s) la Atabatu Abbasiyya tukufu katika mji wa Najafu, mbele ya wasomi waliobobea katika mambo ya Afrika kutoka vyuo vikuu tofauti, pamoja na kundi la wanafunzi wa Dini kutoka bara la Afrika”.
Akaongeza kuwa: “Nimeongoza kikao cha nadwa kwa kushirikiana na mkuu wa wahariri wa jarida la (Dirasaati-Afriqiyyah) Dokta Swabahu Mahadi Ramidhu na Dokta Sarhani Ghulamu, baada ya nadwa tumeandaa maazimio yafuatayo:
- - Kuendeleza mifumo ya tafiti katika Markazi.
- - Kuimarisha uhusiano na vyuo vikuu vya Iraq na kutoa msaada unaohitajika kwa watafiti, na kuwahimiza kuandika maswala ya kitafiki yanayohusu bara la Afrika.
- - Kuboresha jarida la (Dirasaati-Afriqiyyah) na kulifanya kuwa sawa na majarida mengine ya kielimu baada ya kupasishwa hivi karibuni.
- - Kuandika tafiti za wairaq kuhusu Afrika na kuzitangaza kimataifa, ili kituo kisimame kwenye nafasi ya utafiti kimataifa kuhusu Afrika.
- - Kuendelea kufanya nadwa za kujadili bara la Afrika kwa lengo la kuendelea kupata maoni mapya”.
Kumbuka kuwa lengo la nadwa hii ni kuimarisha uhusiano kati ya watafiti wa mambo ya Afrika na Markazi, Atabatu Abbasiyya tukufu itaendelea kusaidia harakati za kielimu na tafiti zinazo husu bara hilo.