Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya amewapa zawadi wanafunzi bora wa shule za Al-Ameed

Maoni katika picha
Kundi la wanafunzi wa shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, wamepewa zawadi na kiongozi mkuu wa kisheria katika Ataba Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi kwenye hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria kwa wavulana iliyofanywa hivi karibuni.

Mjumbe wa kamati kuu katika Atabatu Abbasiyya na msimamizi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya amekutana na wanafunzi walio onyesha vipaji vyao kwenye hafla ya kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria kwa wanafunzi wa shule za Al-Ameed za wavulana”.

Akaongeza kuwa: “Mkutano huu na utoaji wa zawadi unaonyesha namna Atabatu Abbasiyya tukufu inavyojali swala la kuendeleza vipaji vya wanafunzi na kuwataka kuwa mfano mwema kwa wenzao”.

Kumbuka kuwa mkutano huo umehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu pamoja na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: