Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake/ katika mji wa Bagdad chini ya Atabatu Abbasiyya, imeanza semina mpya ya usomaji sahihi na hukumu za tajwidi katika mji wa Kadhimiyya.
Kiongozi wa tawi la Maahadi Ustadhat Anwaar Abdurazaaq amesema: “Kwa baraka za Mwenyezi Mungu mtukufu tumefanikiwa kufungua semina ya Qur’ani ndani ya ukumbi wa Mukhayyamu-Husseiniyya uliochini ya muwakilishi wa Marjaa katika mji wa Kadhimiyya, semina inawashiriki (17) kutoka katika mji wa Kadhimiyya na maeneo Jirani”.
Akabainisha kuwa: “Maahadi bado inaendelea kupokea wanafunzi wapya kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Bagdad, kwa lengo la kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii ya wanawake”.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inafanya kila iwezalo katika kutengeneza kizazi cha wasomi wa Qur’ani wakike.