Kuanza kwa kazi ya kusafisha minara ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wameanza kazi ya kusafisha minara ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kudumisha uzuri wa muonekano wake.

Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Zainul-Aabidina Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi hii imeanza baada ya kumaliza kusafisha kubba takatifu, kazi hii hufanywa kila wakati kwa kufuata ratiba maalum, lakini kunapokua na kimbunga cha vumbi mara kwa mara watumishi wetu nao husafisha kila wakati”.

Akaongeza kuwa: “Kazi huanza juu ya mnara kuja chini, husafishwa sehemu zote za mnara kwa kutumia vifaa maalum visivyo haribu muonekano wa dhahabu”.

Akaendelea kusema: “Kazi hii itafanywa kwa muda wa siku mbili na nusu, tunaanza kufanya kazi nusu ya pili katika siku kutokana na ukubwa wa joto na kuchemka kwa vifuniko vya dhahabu”.

Kumbuka kuwa kutokana na kubadilika hali ya hewa na kusababisha kuchafuka kwa vifuniko vya dhahabu vilivyopo kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hulazimika kufanyiwa usafi kila wakati ili kulinda uimara wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: