Mradi wa Arshu-Tilawa unaendelea na vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Mahafali za usomaji wa Qur’ani zinazoratibiwa na kituo cha miradi ya usomaji wa Qur’ani, chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, zinaendelea kila siku ya Ijumaa jioni kupitia mradi wa Arshu-Tilawa.

Mradi umepata muitikio mkubwa, wahudhuriaji wamesikiliza Qur’ani kutoka katika nyumba aliyoruhusu Mwenyezi Mungu atajwe humo jina lake, iliyosomwa na Liith Al-Ubaidi kutoka Atabatu Abbasiyya na Ahmadi Jamali kutoka mkoa wa Dhiqaar, sambamba na msomaji kutoka mradi wa kiongozi wa wasomaji bwana Abdullahi Mussawi.

Kikao cha usomaji wa Qur’ani kimehudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru na wapenzi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu, pamoja na wahudumu wa kituo, katika mazingira mazuri kiroho yaliyojaa utajo wa Mwenyezi Mungu na mapenzi ya Ahlulbait (a.s).

Kumbuka kuwa kituo cha miradi ya Qur’ani kinaharakati nyingi za Qur’ani, ukiwemo mradi huu wa Arshu-Tilawa, unaolenga kunufaika na vipaji vya wasomaji wa Qur’ani waliopo Iraq, na kuvionyesha katika ulimwengu wa kiislamu, Pamoja na kuendeleza vipaji hivyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: