Idara ya shule za Alkafeel za Dini upande wa wasichana chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefungua semina za ibada ya Hija na Umra kwa wanafunzi wake, kwa ajili ya kuboresha kiwango cha kuzitambua ibada hizo na hukumu zake.
Kiongozi wa idara bibi Bushra kinani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hizi ni miongoni mwa semina za kielimu ambazo hufanywa na idara yetu, huwa tunafundisha ibada mbalimbali ikiwemo Hija na Umra, kutokana na umuhimu wake hasa kwa wasichana, huhitaji kuzifahamu ibada hizo kwa kina”.
Akaongeza kuwa: “Semina itadumu kwa muda wa mwaka mzima, watasoma siku mbili kwa wiki, kwenye kumbi za madarasa zilizopo katika jingo la Swidiqatu-Twahirah (a.s), katika mkoa wa Karbala”.
Akabainisha kuwa: “Tumeandaa selebasi maalum kwa ajili ya semina hiyo, inasimamiwa na msomi aliyebobea mwenye uzowefu mkubwa katika sekta hiyo, idara imeandaa kila kitu kinacho hitajika, kama vile, kumbi za madarasa, vifaa vya kusomea, usafiri na waangalizi wa watoto kwa washiriki watakao kuja na watoto wadogo”.
Akamaliza kwa kusema: “Usajili bado unaendelea, kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba (07707098821) namba hiyo pai inapatikana kwenye whatssap na telegram”.