Kuanza kwa program za msimu wa utamaduni kwa wanafunzi wa sekondari msimu wa joto

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuanza kwa program ya (Msimu wa maarifa ya utamaduni), kwa wanafunzi wa sekondari (upili) katika mkoa wa Karbala, inalenga kunufaika na kipindi cha likizo za majira ya joto, program hii husaidia kuongeza maarifa kwenye mambo tofauti.

Mkuu wa kituo bibi Sara Haffaar ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huu ni muendelezo wa awamu iliyopita, ambayo idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walinufaika, hivi sasa tunafungua awamu hii kwa ajili ya kunufaika na kipindi cha likizo za majira ya joto, vipengele vyote vya program hii vinalenga kujenga maarifa kwa washiriki”.

Akaongeza kuwa: “Program imefunguliwa kwa muhadhara elekezi usemao (Hatua za mafanikio), uliotolewa na muelekezaji Zahara Fadhili, akaongea umuhimu wa mafanikio na mbinu muhimu za kupata mafanikio, akasema kuwa njia ya mafanikio imejaa vikwazo, inabidi mtu uwe na msimamo wa kusonga mbele na kutokata tamaa hadi ufike kwenye malengo yako”.

Akabainisha kuwa: “Miongoni mwa program hiyo kulikua na mhadhara unaohusu mambo ya afya, umetolewa na Dokta Ghazwa Tamimi, ameongea mambo ya kitabibu na afya itokanayo na mlo, sambamba na mihadhara hiyo kulikua na ratiba zingine, kama vile ratiba ya michezo, mashindano na kazi za mikono”.

Kumbuka kuwa program ya (msimu wa maarifa ya utamaduni) kwa wanafunzi ni miongoni mwa program ambazo hufanywa na kituoa, hupata idadi kubwa ya washiriki, jambo hilo limewasukuma wasimamizi kufanya ratiba hiyo mfululizo, na kuweka kila kitu kinachoweza kumnufaisha mshiriki na kuboresha Maisha ya familia katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: