Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Zainul-Aabidina Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumeanza kusafisha kwenye kubba tukufu na minara ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na sehemu zote za paa la haram tukufu, nayo ni miongoni mwa kazi kubwa inayofanywa na kitengo chetu, inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyotokea hivi karibuni, imebidi tufanye usafi mara kwa mara”.
Akaongeza kuwa: “Kazi hii inalenga kulinda paa lisiharibike, tumeanza kusafisha eneo la karibu na kubba na minara mitukufu, hadi kwenye paa la haram na paa la uwanja wa haram pamoja na maeneo yanayozunguka sehemu hiyo, sehemu zinazo safishwa ni:
- - Paa la haram tukufu.
- - Kubba za haram tukufu.
- - Sehemu za katikati ya kubba na hema za vyoo.
- - Mfumo wa viyoyozi kwa nje.
- - Mabango ya majina ya milango ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
- - Kupangilia baadhi ya maeneo.
- - Kukarabati mifumo ya tahadhari za majanga”.
Akabainisha kuwa: “Tumeanza kufanya kazi hiyo baada ya swala ya Alfajiri, ili kuhakikisha wakati wote wa mchana viyoyozi havizimiki, tunafanya kazi kwa umakini mkubwa na kuhakikisha hatusababishi usumbufu kwa mazuwaru”.
Akamaliza kwa kusema: “Tunatumia vifaa maalum vya usafi, visivyo sababisha athari yeyote”.