Wajumbe kutoka shirika la (NORIKA) linalo husika na uzalishaji wa chakula na shirika la (GRIMME) linalohusika na kilimo cha viazi mbatata, ambayo ni mashirika ya Ujerumani, wakiongozana na wajumbe kutoka shirika la Naharu-Auraad ambao ni bwana Shabani Nahari na Abbasi Radhwi, wametembelea mradi wa Firdaus uliochini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wakiwa na mjumbe wa kamati kuu bwana Kadhim Abadah, wametembelea sehemu zote za mradi na eneo la kilimo cha viazi mbatata.
Mkuu wa shirika la Liwaaul-Alamiyya Mhandisi Aadil Maliki ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mafanikio makubwa yamepatikana kwenye mradi wa Firdaus ndani ya miaka miwili iliyopita, tumezalisha kiwango kikubwa cha viazi mbatata pamoja na changamoto zilizokuwepo, jambo ambalo limepelekea mradi wetu kuwavutia watu na mashirika kutoka ndani na nje ya Iraq wanaokuja kuangalia mafanikio ya kilimo cha jangwani, ukiwemo ugeni huu”.
Akaongeza kuwa: “Ugeni umeangalia vifaa vinavyotumika kwenye kilimo pamoja na changamoto na mafanikio ya mradi, wakabaini kuwa mafanikio ni makubwa kushinda changamoto, ukizingatia kuwa kila kazi haikosi changamoto, lakini mafanikio yanapokua juu ndiyo huangaliwa, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, na juhudi za wataalamu wa kilimo hiki likiwemo shirika la Nahari-Auraad”.
Mhandisi Maliki akasisitiza kuwa: “Wageni wameridhika na walichoshuhudia, wameangalia mradi wote pamoja na uongozi wake, mradi umefanikiwa kushinda changamoto, wamesema kuwa mradi huu ni kielelezo cha maendeleo makubwa ya sekta ya kilimo hapa Iraq”.