Baabil imeshuhudia ushiriki wa wanafunzi elfu tisa kwenye mradi wa semina za Qur’ani za majira ya joto

Maoni katika picha
Zaidi ya wanafunzi elfu tisa kutoka mkoa wa Baabil wanashiriki kwenye mradi wa semina za Qur’ani katika majira ya joto, unaoendeshwa na tawi la Maahadi ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya katika mji wa Baabil.

Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinafanywa kwenye wilaya na vitongoji vya Baabil, kama sehemu ya kunufaika na likizo za majira ya joto, miongoni mwa masomo wanayofundishwa ni (Kuhifadhi Qur’ani, Aqida, Fiqhi, Akhlaqi na Sira) pamoja na maarifa ya tamaduni.

Tambua kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Baabil, hufanya harakati mbalimbali za Qur’ani tukufu, pamoja na semina za Qur’ani endelevu.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya chenye jukumu la kufundisha Qur’ani tukufu na kuandaa jamii yenye uwelewa wa Qur’ani katika kila sekta.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: