Zaidi ya wanafunzi elfu 8 wanashiriki kwenye semina za Qur’ani za majira ya joto jijini Bagdad

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Bagdad imesajili wanafunzi zaidi ya elfu nane kwenye mradi wa semina za Qur’ani za kipindi cha likizo za majira ya joto.

Asilimia kubwa ya wanafunzi wanatoka katika vitongoji vya Karkhi na Raswafa, wakufunzi wa semina hizo wapo zaidi ya (250).

Tambua kuwa mradi wa semina za Qur’ani majira ya joto hushiriki zaidi ya wanafunzi elfu (25) kutoka mikoa tofauti ya Iraq, Karbala, Najafu, Bagdad, Baabil, Diwaniyya na Muthanna.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajukumu la kufundisha Qur’ani na kuandaa jamii ya wasomi wazuri wa Qur’ani tukufu katika kila sekta.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: