Kituo cha kiislamu na tafiti za kimkakati chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na Atabatu Radhawiyya, kimefanya nadwa ya kwanza ya kielimu yenye anuani isemayo (Turathi za maneno ya Imamu Ridhwa -a.s-).
Kituo kimemkaribisha Allamah Shekhe Najmu-Dini Twabasi kwenye nadwa ya kwanza, maudhui ya mada yake ilikua inasema (Nadwa kuhusu Imamu Ridhwa a.s).
Baada ya utangulizi mfupi alioongea kuhusu utume katika mapokezi sahihi, akaongea mada ya utakasifu (umaasumu), akaanza kusherehesha yaliyopokewa kutoka kwa Imamu Ridhwa (a.s), kutoka kwenye kitabu cha Ihtijaaj cha Shekhe Twabasi, kipengele cha majibu kwa Ma-amun Abbasi katika baadhi ya mambo”.
Akahitimisha kwa kuhimiza kujali kitabu cha Ihtijaaj, akawaomba wanachuoni wa kiislamu wafuate maelekezo kutoka kwa Maimamu (a.s).
Nadwa imehudhuriwa na wanafunzi wa hauza ya Qum tukufu, na wengine wameshiriki kwa njia ya mtandao.
Tambua kuwa kituo cha kiislamu na tafiti za kimkakati chini ya kitengo cha utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hufanya nadwa za kielimu wakati wote wa mwaka.