Watumishi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafanya maandalizi ya mwisho ya hafla ya kuhitimisha maswala ya malezi, katika shule za awali za Al-Ameed, itakayo fanyika kesho asubuhi.
Rais wa kitengo hicho Dokta Ahmadi Swabihi Kaabi amesema: “Shule za Al-Ameed hufanya hafla kubwa kila mwaka inayohusu maswala ya malezi kwa wanafunzi wake wa awali, kupitia program ya (Nahwul-Qamaru)”.
Akaongeza kuwa: “Watoto watafanya mambo mbalimbali waliyo fundishwa ikiwa ni pamoja na maigizo katika kuonyesha wazazi wao kuwa wako tayali kuingia shule ya msingi”.
Akaendelea kusema: “Program ya (Nahwul-Qamaru) ni program ya kielimu na kimalezi iliyo andaliwa rasmi kwa shule za awali za Al-Ameed, inahusu mambo mengi yanayofundishwa kwa watoto hao, malezi, Dini, utamaduni na mambo mengine yatakayo wasaidia katika maisha yao ya baadae”.