Hatua za kwanza za brogram za watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi na kamati ya utendaji zimeandaa program maalum kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo imezinduliwa kwenye mkutano mkubwa uliofanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Ataba tukufu, na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya marais wa vitengo na wasaidizi wao.

Mjumbe wa kamati tendaji Ustadh Karaar Hussein Maamuri amesema: “Mkutano huo umefafanua mikakati na malengo ya program hiyo, kutoka kwa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya, rais wa kamati ya usimamizi Sayyid Lithi Mussawi, mjumbe wa kamati Dokta Muhammad Hassan Jaabir na rais wa kitengo cha Majmaa ya Qur’ani Dokta Mustaqu Ali”.

Akaongeza kuwa: “Kwenye mkutano huo umetolewa ufafanuzi kamili wa ratiba itakayodumu kwa muda wa siku tano, ratiba hiyo imesheheni maswala ya kitamaduni, masomo ya Aqida, michezo na kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu na mambo mengine mengi, aidha kutakua na mashindano mbalimbali kwa lengo la kukuza vipaji vya washiriki na washindi watapewa zawadi, kulingana na kila aina ya shindano”.

Akamaliza kwa kusema: “Program inaangalia pia idadi ya watumishi katika kila kitengo, ili isiathiri utendaji wa kazi kwenye vitengo vya Ataba tukufu, sambamba na kugawa majukumu kwa kila kitengo kinacho shiriki, kwani hii ni program jumuishi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: