Idara ya Habari chini ya kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeweka zaidi ya mabango 70, kwa ajili ya kujiandaa na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s), aliyezaliwa mwezi kumi na moja Dhulqaada.
Rais wa kitengo tajwa Sayyid Naafi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kitengo huanza kuweka mazingira ya furaha katika kumbukumbu za kuzaliwa kwa Imamu miongoni mwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s), ikiwa ni pamoja na eneo hili tukufu la katikati ya malalo mawili Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi (a.s), watumishi wa kitengo chetu wamefanya kazi tofauti ya kuandaa mazingira ya maadhimisho haya”.
Akaongeza kuwa: “Idadi ya mabango yaliyowekwa ni zaidi (70), yamewekwa juu ya nguzo za taa zilizopo kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili, yameandikwa maneno ya pongezi kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w), na kuonyesha furaha waliyonayo Ahlulbait (a.s) na wafuasi wao”.
Mussawi akabainisha kuwa: “Tunaweka mazingira haya kwa ajili ya kuwafanya mazuwaru wahisi tukio hili, ambalo ni sehemu ya kufanyia kazi kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo: (Huisheni mambo yetu.. Mwenyezi Mungu amrehemu atakaehuisha mambo yetu).
Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimeandaa ratiba maalum kwa ajili ya kuadhimisha tukio hili siku ya Jumamosi (11 Dhulqaada), inamambo mbalimbali yatakayo fanywa katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.