Sayyid Swafi amshukuru mlezi wa kijana wa Marjaiyya mkuu na familia za mashahidi na majeruhi

Maoni katika picha
Ratiba ya kuhitimisha program ya (Nahwul-Qamaru) inayohusu watoto wa shule za Al-Ameed, inayosimamiwa na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inamaigizo tofauti yanayofanywa na watoto wa shule za awali, wameonyesha kila walicho fundishwa na walimu wao kwa ajili ya kuingia shule ya msingi.

Miongoni mwa maigizo waliyofanya ni igizo la kuonyesha namna raia wa Irar walivyo jitokeza kuitikia fatwa ya Marjaa Dini mkuu ya kulinda Iraq na maeneo matakatifu.

Baada ya igizo hilo Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi alitoa shukrani kwa Marjaa Dini mkuu na fatwa yake tukufu, iliyolinda ardhi ya Iraq na maeneo matakatifu, sambamba na kushukuru familia za mashahidi na majeruhi zilizojitolea kila kitu kwa ajili ya taifa hili tukufu, akapongeza juhudi zinazofanywa na shule za Al-Ameed kwa malezi bora wanayotoa kwa vijana hawa”.

Kumbuka kuwa wanafunzi wamefanya maigizo ya aina tofauti, likiwemo igizo la mazingira ya kutolewa fatwa na Marjaa-Dini mkuu, na jinsi fatwa hiyo ilivyolinda taifa la Iraq na maeneo matakatifu sambamba na kusaidia familia za mashahidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: