Mtandao wa kimataifa Alkafeel (url=https://alkafeel.net/ar-news/control/) unatoa wito kwa wapenzi wa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) koto duniani, kusajili majina yao kwa ajili ya kufanyiwa ziara kwa niaba mbele ya kaburi la Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) katika mji wa Mash-hadi, katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (a.s), kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara.
Idara inayosimamia jukumu la kufanya ziara kwa niaba imesema: kila mtu atakaesajili jina lake, atafanyiwa ziara na kuombewa dua ndani ya haram ya Imamu Ridhwa (a.s) pamoja na swala ya ziara.
Kumbuka kuwa kufanya ziara kwa niaba ni moja ya huduma muhimu inayotolewa na watumishi wa idara ya teknolojia na taaluma kupitia mitandao ya Atabatu Abbasiyya tukufu iliyochini ya mtandao rasmi wa kimataifa (Alkafeel).