Sayyid Swafi amekutana na kundi la mayatima wenye vipaji na amewahimiza kuendeleza vipaji vyao

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi Alasiri ya leo siku ya Ijumaa, amekutana na kundi la mayatima waliokatika mradi wa (dhibiti kipaji) hatua ya pili.

Mkuu wa kamati tendaji ya mradi huo, Ustadh Omari Ula Alkifai ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kikundi hiki ni washiriki wa kwanza katika mradi wa wenye vipaji, unaoendelea hivi sasa kupitia mihadhara, warsha, mashindano na ziara, miongoni mwa ratiba zake wamekutana na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, mlezi na mfadhili wa kwanza wa mradi huu”.

Akaongeza kuwa: “Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ameangalia vipengele vya hatua ya kwanza na inayofuata katika mradi huu, akaangalia mafanikio yaliyopatikana”.

Akafafanua kuwa: “Amesikiliza na kushuhudia vipaji walivyonavyo vijana hao, na mambo watakayo fanyiwa na mradi wa (Dhibiti kipaji) katika kuendeleza vipaji vyao”.

Akabainisha kuwa: “Mwishoni mwa mkutano Sayyid Swafi amesisitiza kuongeza juhudi katika safari ya masomo sambamba na kuendeleza vipaji vyao kupitia mradi huu mtukufu, akasifu kazi nzuri inayofanywa na idara ya mradi na kitengo cha uhusiano pamoja na wote wanaoshirikiana nao”.

Kumbuka kuwa mradi huu ni wa aina yake hapa Iraq, unasehemu mbili, kwanza ni kubaini vipaji na kuviendeleza kwa kushirikiana na taasisi za kiraia, na sehemu ya pili ni kusaidia vijana wenye vipaji adimu, umekua na mafanikio makubwa yanayo endana na malengo ya mradi na hali halisi tunayo ishi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: