Daru-Rasuulul A’adham (s.a.w.w) inaendelea kufanya harakati za kongamano la Siratu-Nnabawiyya

Maoni katika picha
Daaru-Rasuumul A’adham (s.a.w.w) chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na shughuli za kongamano la Siratu-Nnabawiyya baada ya kufanya nadwa za kielimu.

Akaongeza kuwa: “Dokta Jawadu Ali ni mmoja wa wanahistoria mashuhuri wa kiarabu katika zama hizi, kutokana na vitavu alivyo andika, kama vile kitabu cha (Historia ya waarabu kabla ya uislamu), na vitabu vingine alivyo andika, nadwa hii inaangazia vitabu rejea alivyo tegemea wakati wa kusoma kwake historia, na matokeo mapya aliyopata na namna ya kuendana na mazingira yenye kuathiri wakati wa kuandika historia ya Mtume”.

Akabainisha kuwa: “Kuna maarifa makubwa kwa Jawadi Ali na uchambuzi wa turathi za kiarabu, sambamba na changamoto za uandishi wa historia ya uislamu, alihitimu masomo ya juu na kupata shahada ya udaktari nchini Ujerumani, katika miaka ya thelathini karne iliyopita, amefundisha katika vyuo vikuu vikubwa vya kiarabu na kimataifa”.

Akafafanua kuwa: “Dokta Jawadu Ali alianza kazi ya kuandika historia ya waarabu kabla ya uislamu miaka ya sitini, akafanikiwa kuandika historia ya Mtume kwenye kitabu kilicho toka mwaka (1961) kwa jina la (Historia ya waarabu katika uislamu na Siratu Nabawiyya)”.

Kumbuka kuwa malengo makuu ya kufanya makongamano haya matukufu ni kuhamasisha wasomi wa vyuo vikuu na hauza kuandika vitabu vya historia, na kutaja changamoto zilizotokea katika historia na namna ya kuzitatua kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: