Wanafunzi wa mradi wa semina za Qur’ani majira ya joto wanaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ridhwa (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, asubuhi ya leo siku ya Jumamosi, imefanya hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ridhwa (a.s) kwa wanafunzi wa mradi wa semina za Qur’ani majira ya joto unaoendelea hivi sasa.

Hafla hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa jengo la Al-Ameed na kuhudhuriwa na rais wa Majmaa ya Qur’ani tukufu Dokta Mushtaqu Ali, mkuu wa Maahadi na baadhi ya viongozi, pamoja na wanafunzi wanaoshiriki kwenye mradi.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na mmoja wa wanafunzi wa Mradi, kisha wakaanza kuimba kaswida za kuwasifu watu wa nyumba ya Mtume (a.s) hasa muadhimishwa aliyezaliwa siku kama ya leo mwezi kumi na moja Dhulqada mwaka 148h.

Ratiba ya hafla hiyo ilikua na kipengele cha kugawa maua ya pongezi na pipi, sambamba na kuambiana maneno mazuri ya pongezi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: