Atabatu Abbasiyya inafanya hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ridhwa (a.s)

Maoni katika picha
Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) jioni ya siku ya Jumamosi, imefanyika hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s), Imamu wa nane katika Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s)

Hafla hiyo imehudhuriwa na idadi kubwa ya viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kundi la mazuwaru, ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Liith Ubaidi,

Ukafuata mhadhara kutoka kwa Shekhe Aadil Wakiilm makamo rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, ameanza kwa kutoa pongezi kutokana na tukio hili, akaeleza hatua muhimu za Maisha ya Imamu Ridhwa (a.s), kuanzia kuzaliwa kwake na malezi aliyopata katika nyumba ya baba yake Imamu Alkadhim (a.s), na hadithi zilizo pokewa kuhusu utukufu wake, safari yake ya kutoka katika mji wa babu yake, mji wa Madina na kuelekea Khurasani kwa amri ya Ma-amun Abbasi, elimu kubwa aliyokua nayo (a.s), mchango wake kwa umma wa kiislamu na thawabu anazopata mtu anayekwenda kumtembelea katika ardhi ya ugenini aliko zikwa.

Kisha wahudhuriaji wakamswalia mtume kwa sauti za juu, zilizojaa furaha, halafu mashairi mazuri kuhusu kumbukizi hii yakasomwa na washairi wafuatao: Sayyid Muhammad Yaasiri, Muhammad Twalibu, Zainul-Aabidina Saidi wakahitimisha kwa utenzi uliosomwa na Muhammad Amiri Tamimi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: