Kufanyika kwa hafla za mimbari Nuru katika mji wa Diwaniyya kwa ushiriki wa wasomi wa kimataifa

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya mahafali ya usomaji wa Qur’ani kupitia mradi wa mimbari za nuru katika makao makuu ya Mkoa Alqadisiyya (Diwaniyya), kwenye wilaya ya Afaku, kwa ushiriki wa wasomi wa kimataifa kutoka ndani na nje ya Iraq, ndani ya ukumbi wa Husseiniyyatu-Nnabii A’adham (s.a.w.w).

Hafla ya usomaji wa Qur’ani imefanywa katika mazingira mazuri, masikio ya wahudhuriaji yalianza kuburudishwa na msomaji wa Ataba mbili tukufu Sayyid Hassanaini Halo, na msomaji wa kimataifa Karim Mansuri kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Iran, halafu msomaji wa Ataba mbili tukufu bwana Liith Ubaidi akasoma pia.

Mahafali imepambwa na mashairi yaliyojaa beti za kuhimiza kuvipenda vizito viwili kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume (s.a.w.w), yaliyosomwa na muendeshaji wa hafla (mc) bwana Hassanaini Jazairiy, aliongea maneno mazuri zaidi ya kuisifu Qur’ani na watu wa nyumba ya Mtume (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: