(Makaburi ya pamoja raia chini ya udongo) anuani ya kitabu kilichoandikwa kwa lugha tatu

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha kiiraq cha kuthibitisha jinai za magaidi chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa kitabu kipya kiitwacho: (Makaburi ya pamoja raia chini ya udongo), kwa lugha tatu, kiarabu, kiengereza na kifaransa.

Mkuu wa kituo hicho Dokta Abbasi Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kitabu hiki ni sehemu ya kuonyesha jinai zilizofanywa na magaidi, kituo kimekua kikiandika jinai hizo kwa lugha tofauti, machapisho yote tunayotoa yanalenga kuonyesha jinai zilizofanywa na magaidi”.

Akaongeza kuwa: “Kitabu kinapicha za makaburi ya pamoja ya watu waliouawa na utawala uliopita, makaburi yaliyozikwa mamia ya watu katika mikoa tofauti ya Iraq, yanaonyesha kilele cha dhulma na mateso ambayo raia walipitia katika kipindi hicho”.

Kumbuka kuwa kituo cha Iraq cha kuthibitisha jinai za magaidi kinawajibu wa kuonyesha jinai walizofanyiwa raia wa Iraq, tunakusanya taarifa zote na kuzithibitisha kwa picha, kuanzia lilipoanzishwa taifa la Iraq hadi sasa, tumesha toa machapisho mengi na vitabu tofauti.

Kupakua kitabu hicho, chenye lugha tatu tumia link ifuatayo:

https://iraqicenter-fdec.org/archives/category/publications

Kwa anayetaka kukiona atembelee maonyesho ya vitabu vya Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: