Idara ya Tahfiidh inaendesha ratiba maalu ya masomo ya kipindi cha joto kwa wanafunzi wake

Maoni katika picha
Ratiba ya masomo ya majira ya joto inayosimamiwa na idara ya Tahfiidh chini ya Maahadi ya Qur’ani imeanza semina za majira ya joto, zinazolenga kuongeza kiwango cha uhifadhi na kudhibiti walicho hifadhi awali.

Ratiba hii itadumu kwa muda wa miezi mitatu, watafundishwa masomo tofauti, jumla ya wanafunzi (40) kutoka mkoa wa Karbala wanashiriki kwenye ratiba hiyo.

Kila siku hutolewa mihadhara, kuna kupindi cha michezo na wakati wa mapumziko, aidha Maahadi inagawa chakula kwa wanafunzi wake.

Ratiba hii inahusisha safari za kwenda kutembelea malalo takatifu na Maraajii-Dini watukufu katika mji wa Najafu, sambamba na kutoa zawadi kwa wanafunzi watakao fanya vizuri.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani kupitia matawi yake, ni moja ya vitua vya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inajukumu la kufundisha Qur’ani na kuandaa jamii yenye uwelewa wa Qur’ani katika kila sekta.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: