Wanafunzi elfu 4 wamejiunga na mradi wa semina za Qur’ani za majira ya joto katika wilaya ya Hindiyya

Maoni katika picha
Wilaya ya Hindiyya imeshuhudia mwitikio mkubwa wa wanafunzi kwenye semina za Qur’ani za majira ya joto, zinazo endeshwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu, wanafunzi waliosajiliwa kwenye mradi huu ni zaidi ya (4000).

Wanafunzi wamegawanyika sehemu (80), misikitini, kwenye Husseiniyya pamoja na baadhi ya maeneo ya walimu vijijini.

Tawi la Maahadi katika wilaya ya Hindiyya linafikisha huduma za Qur’ani kwa wanafunzi wake wote, kwa lengo la kuhakikisha wananufaika na kipindi cha likizo za majira ya joto, sambamba na kuongeza kiwango cha maarifa ya Dini.

Walimu wanaofundisha Qur’ani kwenye mradi huo katika wilaya wa Hindiya wamefika (92), wanafundisha kusoma Qur’ani, kuhifadhi, Aqida, Fiqhi, Akhlaqi na Sira.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya vituo vya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inajukumu la kufundisha Qur’ani tukufu na kuandaa kizazi chenye uwelewa wa Qur’ani katika sekta zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: