Kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimehitimisha nadwa za kitaalamu zilizofanywa kwa kushirikiana na Atabatu Radhwawiyya tukufu.
Katika nadwa ya mwisho kituo kimemkaribisha Dokta Imdadi Torani, aliyetoa mada isemayo: (Tauhidi mbele ya Imamu Ridhwa a.s).
Dokta Torani akaeleza riwaya zilizopokewa kutoka kwa Imamu Ridhwa (a.s) katika maudhui ya tauhidi, sambamba na kutaja riwaya zingine kutoka kwake (a.s).
Akahitimisha mada yake kwa kutaja nafasi kubwa aliyokuanayo Imamu Ridhwa (a.s) katika umma wa kiislamu, na mazungumzo yake na makundi mengine.
Mwishoni mwa kikao kukawa na maswali kutoka kwa wanafunzi wa hauza walioshiriki kwenye nadwa hiyo kwa kuhudhuria moja kwa moja na kwa njia ya mtandao, mtoa mada amejibu maswali yote na kutoa ufafanuzi zaidi.
Kumbuka kuwa kituo kipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu.