Waziri wa mazingira katika ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Waziri wa mazingira Dokta Jasim Abdul-Azizi Hamadi ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu akiwa na wajumbe aliofuatana nao.

Wamefanya ibada ya ziara na kusoma dua mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha wakafanya kikao na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi na viongozi wengine.

Baada ya kukaribishwa wageni hao, ambao wamefuatana na mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswifu Jaasim Alkhatwabi, wamejadili mambo mengi, ikiwa ni pamoja na huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru, na mchango wake katika kutunza mazingira, aidha wameangazia baadhi ya miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu inayosaidia swala zima la utunzaji wa mazingira na hali halisi ya mazingira iliyopo sasa hapa nchini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: