Hatua ya mwisho ya kuweka vioo kwenye kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kazi ya kuweka vioo kwenye kubba la malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani, imefika hatua ya mwisho, kazi hiyo inafanywa na watumishi wa kitengo cha ujenzi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Msimamizi mkuu wa kazi hiyo na kiongozi wa idara ya vioo Sayyid Hassan Saidi Mahadi amesema: “Hii ni kazi kubwa kufanywa kwa utaratibu huu tangu miaka ya tisini karne iliyopita, hii ndio hatua ya mwisho katika uwekaji wa vioo kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwenye paa na kuta zake, chini ya utaratibu uliopangwa sambamba na kuweka mapambo yanayoendana na yale yaliyopo kwenye ukumbi wa haram takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Mapambo yanayowekwa ni nakshi za kiislamu zinazo fanana na zilizokuwepo zamani, pamoja na kuweka baadhi ya urembo mpya, vioo vinavyo wekwa ni imara na vinawekwa kwa umakini na umaridadi mkubwa”.

Akamaliza kwa kusema: “Pamoja na kusimama simama kwa kazi katika vipindi vya ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ukizingatia kuwa sehemu ya mradi inazunguka dirisha takatifu, na kazi za ujenzi zinatatiza mazuwaru watukufu, lakini tayali tupo katika hatua ya mwisho na kazi imefanywa kama ilivyo pangwa, mafundi wetu wamefanya kazi kubwa katika kufanikisha ujenzi huu kwa ufanisi mkubwa”.

Tambua kuwa kazi hii ni sehemu ya ukarabati na uendelezaji wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), inafanywa kwa utaratibu maalum unaoendana na utukufu wa eneo hili na athari yake.

Kumbuka kuwa kazi zote zinazofanywa na watumishi wa kitengo cha usanifu na ufundi, ni kielelezo cha kujitegemea kwenye fani za uhandisi, kazi inaendelea bila kusimama wala kuzuwia harakati za mazuwaru, kazi hugawanywa sehemu tofauti na hupangwa zamu za watumishi kwa nyakati tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: