Inatokea hivi sasa.. kuanza kwa kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya sita

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo siku ya Alkhamisi ndani ya ukumbu wa Imamu Hassan (a.s), vimeanza vikao vya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya sita chini ya kauli mbiu isemayo: (Marjaa-Dini ni ngao ya umma wa kiislamu).

Hafla ya ufunguzi wa kongamano litakalodumu kwa muda wa siku mbili imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katibu mkuu, makamo katibu mkuu, wajumbe wa kamati kuu, marais wa vitengo, viongozi wa idara, wawakilishi wa serikali ya mkoa wa Karbala, viongozi wa Dini, na viongozi wa idara za ulinzi na usalama.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Sayyid Hassanain Halo, kisha ikasomwa surat Faat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Ibaa).

Ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kisha likasomwa shairi na Dokta Haazim Rashaki Tamimi.

Ikaonyeshwa filamu maalum inayomuhusu Marjaa-Dini mkuu Sayyid Sastani na Shekhe Fat-hu Llahi Asfahani, halafu kikazinduliwa kitabu kinachoeleza mauaji ya Spaikar.

Kisha ratiba ya kongamano ikaendelea na Mheshimiwa Shekhe Hussein Aali Yaasini akawasilisha mada yake.

Tunatarajia ratiba itaendelea tena leo Alasiri ikiwa na mada kuu isemayo: (Kuitikia fatwa takatifu: wawakilishi wa Marjaa na vyombo vya Habari mifano hai), kisha kitafuata kikao cha usomaji wa Qur’ani, kitafanywa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na hapo zitahitimishwa shughuli za kongamano hili katika siku ya kwanza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: