Jioni ya Alkhamisi imefanywa hafla ya usomaji wa Qur’ani ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni sehemu ya shughuli za siku ya kwanza katika ratiba ya kongamano la kukumbuka fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya sita.
Hafla imeratibiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na Muhammad Ridhwa Zubaidi, akafuata Liith Ubaidi na kuhitimisha kwa usomaji wa Ali Saidi, imepambwa na mashairi kutoka kwa muendesha hafla (m.c).
Mazuwaru wameshiriki kwenye hafla hiyo, wamekaa wanasikiliza Qur’ani na kutafakari aya zake, zilizokua zinasomwa katika mazingira hayo tulivu.
Kumbuka kuwa hafla hiyo ilikua inahitimisha ratiba ya siku ya kwanza ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda, iliyoanza leo siku ya Alkhamisi asubuhi chini ya kauli mbiu isemayo: (Marjaa-Dini ni ngao ya umma wa kiislamu), linalenga kuadhimisha fatwa ya Marjaa-Dini mkuu ya kulinda Iraq na maeneo matakatifu, hafla ya Qur’ani ni moja ya vipengele vyake.