Kwa ushiriki wa kiongozi mkuu wa kisheria.. Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa zawadi kwa familia za mashahidi wa mauaji ya Spaikar

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa zawadi kwa familia za mashahidi wa Spaikar mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, kwenye hafla ya kuhitimisha kongamano la fatwa tukufu ya kujihami awamu ya sita, iliyofanywa jioni ya leo siku ya Ijumaa.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo, Sayyid Aqiil Abdulhussein Alyaasiri amesema: “Atabatu Abbasiyya imetoa zawadi kwa familia za mashahidi wa mauaji wa Spaikar mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria na katibu mkuu, sambamba na kukumbuka familia zote za mashahidi wa Iraq, waliojitolea wazazi wao, watoto wao na ndugu zao kwa ajili ya kulinda taifa la Iraq na maeneo matakatifu dhidi ya magaidi wa Daeshi”.

Akaongeza kuwa: “Kamati ya maandalizi imewapa umuhimu mkubwa familia za mashahidi wa Spaikar, walio umiza roho za raia wote wa Iraq, waliuawa vijana wa kiiraq zaidi ya (1700) wasiokua na hatia yeyote, mauaji hayo yalifanywa na magaidi wa Daesh, hakika tukio hilo bado linauma hadi sasa”.

Akabainisha kuwa: “Familia za mashadi tumezigawa kwenye makundi, ili iwe rahisi kufikia familia zote zilizopo kwenye kongamano hili, tutaendelea kufikia familia zingine kwenye makongamano yajayo”.

Familia za mashahidi wa Spaikar zimeshukuru sana Atabatu Abbasiyya kwa kuwakumbuka na kuwapa zawadi, wakasema hilo sio jambo geni kwa Ataba, imekua mstari wa mbele kusaidia familia za mashahidi sambamba na kuwatembelea kila wakati.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya imekua ikisaidia familia za mashahidi na majeruhi wa fatwa tukufu ya kujilinda, walioitikia wito wa fatwa tukufu ya Marjaa Dini mkuu ya kulinda taifa la Iraq na maeneo matakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: